Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Wakati ambao kuna karibu muda mwingi uliobakia hadi kufikia Arbaeen ya Imam Hussein (a.s), Mazuwwari wanaotembea kwa miguu wa Arbaeen ya Imam Hussein (as) wakiongozwa na kauli mbiu: "Kutoka baharini hadi mahali pa kifo cha kishahidi cha Imam Hussein -a.s-) walianza Matembezi hayo katika eneo la 'Ras al-Bisheh' katika Mji wa 'Faw' Kusini mwa Mkoa wa Basra.
Mazuwwari hawa wameshikilia mikononi mwao Bendera Nyeusi, za Kijani kibichi na Nyekundu zilizoandikwa maneno haya: “Labbaika Ya Hussein” na “Labbaika Ya Abbas”.
Masafa ya njia ya Baharini kuelekea Karbala Al-Mualla', sehemu ya palipotokea kifo cha Kishahidi cha Imam Hussein (as) ni Kilomita 500.
Inakadiriwa kuwa kuanza mapema kwa Matembezi ya Arbaeen ya mwaka huu, kwa mwaka huu kumetokana na uwepo wa joto kali la mwaka huu, na hili linamaanisha kuwa itakuwepo hali ya kupumzika na kusimama kwa muda mrefu zaidi njiani.
Idara ya Barabara na Madaraja katika Mkoa wa Baghdad ilitangaza kuzindua kampeni mbili za ujenzi wa njia za Mazuwwari kuelekea Karbala al_Mualla' kutokana na pendekezo la Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia' Al-Sudani.
Iraq inajiandaa kuwakaribisha na kuwapokea Mazuwwari wa Iran na wageni wa nchi zingine katika Marasimu ya Arbaeen.